............................................
Na Mwandishi Wetu,BabatiViongozi na wajumbe wa kamati ya maadili ya Mkoa wa Manyara wameaswa kutenda haki kwenye majukumu yao ya kila siku kwa wananchi na kufanya kazi kwa weledi kama inavyotakiwa.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe.Queen Sendiga, alipokuwa akizungumza na wajumbe hao kwenye hafla ya Uapisho wa viongozi na Wajumbe wa Kamati ya Maadili ya Mkoa na Wilaya zote tano, iliyofanyika Oktoba 24, 2025 katika ofisi ya Mkuu wa mkoa.
"Sasa kwa kuzingatia haya ni lazima tukafanye kazi bila kuonyesha upendeleo wowote, na mimi nikiwa kama mwenyekiti wa kamati ya mkoa nimekula kiapo pia hapa, ambacho nimekula kiapo kwa Mungu na kwa wananchi ambao tutaenda kuwasaidia kwa hiyo ni muhimu sana tukafanye majukumu yetu kwa kuzingatia viapo vyetu, lakini kutanguliza mbele maslahi ya wananchi kwa sababu utoaji wa haki ni jambo muhimu sana." alisema Mhe. Sendiga.
Aidha, ametoa wito kwa wajumbe waliokula kiapo kuwa, dhamana waliopewa waende wakaitendee haki kwa mashahi mapana na Taifa letu. Pia amewaomba wakienda kutekeleza majukumu yao waende wakafanye kwa uaminifu, usiri, jasiri na kutokushawishiwa katika utoaji wa haki ya wananchi ama yeyote atakaekwenda kulalamika.
"Ni matarajio yangu kuwa, kamati hizi za maadili zitakuwa chachu katika kuimarisha na kuleta taswira njema kwa mahakama katika mkoa wetu wa Manyara, pia tukafanye kazi kwa uadilifu." Alisema Mhe.Sendiga.



0 Comments