Muonekano wa dawa za asili za aina mbalimbali katika duka la Dkt. Ibou (HERBAL)
.................................
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
TIBA Asilia imekuwa
nguzo kubwa katika ustawi wa afya za jamii na imekuwa ni kimbilio la watu wengi.
Jitihada kubwa za
tafiti ambazo zimekuwa zikifanywa na waganga wa tiba za asili zimeongeza dawa
za kutibu magonjwa ya aina mbalimbali hivyo kuchagiza uboreshaji wa afya za
wananchi.
Dkt. Yusuph Ibou ni
mmoja kati ya watafiti wa dawa za tiba asili hapa nchini ambaye amegundua dawa
yenye mchanganyiko wa miti sabini inayofanya vizuri katika kutibu magonjwa ya
aina tofautitofauti.
Akizungumza na
waandishi wa habari Dkt. Ibou anasema kupitia tafiti za dawa za asili anazo
zifanya zimekuwa na tija hivyo kuwa kimbilio la watu wenye changamoto
mbalimbali za kiafya.
“Dawa za asili zimekuwa
zikihitajika sana hivyo sisi waganga wa tiba za asili tunapaswa kujidhatiti
kufanya tafiti na kuanzisha viwanda vya kuzalisha dawa zetu hizi za asili
ambazo zinaendelea kukubalika kwa jamii kutokana na ubora wake,” alisema Ibou.
Alisema dawa hizo
wanazozizalisha zimekuwa zikisaidia kuimarisha afya za wananchi hivyo kujenga
taifa lenye maendeleo na kueleza kuwa bila ya kuwepo kwa afya bora hakuna
maendeleo yoyote yatakayoweza kufanyika.
Dkt. Ibou alitaja baadhi ya magonjwa yanayotibiwa na dawa alizozifanyia utafiti kuwa ni malaria
sugu ambayo yana pona kwa siku saba baada ya kuzitumia, Typhoid, minyoo mikubwa na midogo, vidonda vya tumbo
na magonjwa ya ngozi.
Alitaja magonjwa mengine kuwa ni ngiri, maumivu ya viungo, kipanda uso, bawasiri na mengine mengi.
Dkt. Ibou (HERBAL) ofisi yake ipo Barabara ya Nane Msikiti wa Warangi jijini Dodoma na kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0686851664, 0767851664 na 0718858664.
Dkt. Yusuph Ibou akionesha dawa zake alizozifanyia utafiti na kusajiliwa na Serikali.
Dkt. Yusuph Ibou akiwa ofisini kwake Barabara ya Nane karibu na Msikiti wa Warangi Jijini Dodoma.
0 Comments