Na Miza Othman Mkame Maelezo –Zanzibar 14/8/20014.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Idrissa Muslim Hija amewataka wananchi wanaotumia Bandari za Mkoa wa Kusini kuwa na Umoja na Ushirikiano kwa lengo la kulinda usalama ndani ya Mkoa huo.
Ameyaeleza hayo wakati alipokuwa akizungumza na wakuu wa kamati za ulinzi na usalama, Masheha, Manahodha na wamiliki wa vyombo vidogo vidogo vya usafiri wa baharini pamoja na wananchi wa Mkoa huo katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibnar (SUZA) Tunguu.
Amesema Masheha wanajukumu kubwa katika kulinda na kusimamia usalama wa bandari zote zilizomo ndani ya Mkoa huo ili kuhakikisha sheria zilizowekwa zinafuatwa.
“Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA) imeundwa kusimamia Manahodha wa vyombo vya Baharini na kila mmoja anahaki ya kulinda na kuzuia uhalifu usiweze kutokea”, alisema Idrisa Muslim Hija.
Mkurugenzi wa usajili na vyeti Sheikha Juma amesema sheria za kulinda usalama wa bandari zimeshaanzishwa tangu mwaka 2010 kwa hivyo kila raiya analazimika kuzifuate ili kuondosha migogoro isiyo ya lazima.
Amesema hadi hivi sasa wameshaanza kusajili vyombo vidogo vidogo vyenye urefu wa ziraa nane au urefu wa mita nne kwani kufanya hivyo kutapelekea kurahisisha upatikanaji wa chombo cha muhusika wakati anapotokewa na tatizo ikiwemo kupotea, kuungua na hata kuibiwa kwa chombo chenyewe.
“Nilazima raiya atekeleze sheria zilizopo ili kujiepusha na majanga na panapotokea ajali muhusika aweze kulipwa fidia”, alisema Sheikha Juma Mohammed.
Aidha amesema nilazima Manahodha wawe mstari wa mbele kutekeleze sheria za bandari zilizopo kwa lengo la kusaidia Serikali kuipatia mapato ili iweze kujiimarisha kiuchumi.
1 Comments
Works Cited - Paul, S. “ZMA Testosterone Reviews: Benefits, Dosage & Side Effects.” Testosteroneofficial.Com Ie. Testosterone Official, 6 Sep. 2018, https://testosteroneofficial.com/research/zma/.
ReplyDelete