MWENYEKITI wa UVCCM Mkoa wa Ruvuma, Ndugu Kelvin K. Charles, ilikuwa Tar12 Julai 2025 Alikuwa Mgeni Rasmi katika mchezo maalum wa kuchangia watoto wenye mahitaji maalumu, uliowakutanisha timu za RUVUMA COMBINE dhidi ya RUVUMA ALL STARS katika uwanja wa CCM Majimaji, Songea.
Akizungumza baada ya mechi hiyo Ndugu Kelvin k. Charles aliwapongeza waandaaji kwa moyo wao wa kizalendo na kuwahimiza waendelee kuandaa michezo ya aina hiyo kila msimu wa mapumziko, ili kuimarisha mshikamano wa kijamii na kusaidia makundi yenye uhitaji.
Aidha alitoa wito kwa wadau wa maendeleo, mashirika, na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kusaidia watoto na watu wenye mahitaji maalumu.
Pia alisisitiza umuhimu wa ushiriki wa amani, utulivu na uzalendo katika Uchaguzi Mkuu wa 2025, akiwataka vijana na wananchi wote wa Ruvuma kujiandaa kwa nidhamu na mshikamano.
Kwa kuhitimisha Ndugu Kelvin aliahidi kuendelea kuwaunga mkono waandaaji wa matukio ya kijamii kama haya ili kufanikisha dhamira njema ya kuijenga jamii jumuishi.
Katika mchezo huo, RUVUMA COMBINE iliibuka kidedea kwa ushindi wa goli 4-0 dhidi ya RUVUMA ALL STARS.
0 Comments