..................................................
Na Said Hamdsni
Lindi.
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema
kujengwa kwa Bandari ya Uvuvi Wilaya ya Kilwa,mkoani Lindi,kutafungua fursa
mpya ya ajira na kukuza pato la Taifa.
Ulega ameyaeleza hayo wakati anazungumza na
waandishi wa vyombo mbalimbali vya
habari alipotembelea mji mdogo wa Masoko,Wilaya ya Kilwa kuona ujenzi wake.
Waziri amesema ujenzi wa Bandari hiyo
utapokamilika utachochea ukuwaji uchumi
kwa wananchi wa maeneo husika na kukuza pato la Taifa.
Ametaja faida zingine zitazopatikana kupitia
Bandari hiyo ni pamoja na watanzania 30,000 kupata ajira na teknolojia ya
shughuli zitakazoendelea.
Amesema sekta ya uvuvi pekee imeajiri idadi ya watanzania wasiopungua milioni
tano,wakiwemo mmoja mmoja kulingana na mnyororo wa thamani ya sekta hiyo.
Waziri Ulega amesema kukamilika kwa ujenzi wake
itakuwa inapokea na kuweka Nanga Meli kubwa kumi za urefu wa mita 30 na Boti
300 za wavuvi wadogo kwa wakati mmoja.
Amesema ujenzi utapokamilika Bandari itakuwa na
eneo la kuchakata samaki wabichi wavuvi wadogo na soko kubwa la mazao
yanayotokana na Bahari.
Waziri Ulega amesema lengo la Serikali ni kuinua
mikoa yote inayozungukwa na Bahari ya Hindi, Pwani Lindi,Mtwara,Dar es salaam na
Tanga.
Amesema uzinduzi wa ujenzi huo utafanywa na Rais
Dkt Samia Suluhu Hassan Septemba 19 mwaka huu, mji mdogo wa Masoko Wilaya ya
Kilwa.
Bandari ya uvuvi Kilwa inajengwa na kampuni ya
HEC kutoka Jamhuri ya watu wa China kwa gharama ya Sh. Bilioni 262.0 na
utachukua muda wa miezi 36 hadi kukamilika kwake.
Mwanzoni akimkaribisha Waziri Ulega kuzungumza na
waandishi hao,Mkuu wa Wilaya ya Kilwa,Christopher Ngubiagai alisema Kabla ya
nchi yetu haijapata Uhuru kutoka kwa utawala wa kikoloni Kilwa ilikuwa na maendeleo
ya kiuchumi kwa kuwa na Salafu yake.
Ngubiagai alisema kuondoka utawala wa wakoloni
akiwemo Ebuni Matuta miaka ya 1,331 Kilwa imedondoka kiuchumi kutokana na
kukosekana viwanda na taasisi zinazochangia Ajira kwa wananchi.
Amesema kukamilika kwa Bandari hiyo kutaandika
historia mpnz ya kiuchumi ndani ya Wilaya,Mkoa na Taifa.
Wakizungumzia ujenzi wa mradi wa Bandari hiyo
Shaibu Juma,Selemani Serenge,Yusufu Saidi na Elena Mathias wanashukuru kupata
mradi huo kwa madai utapungiza wimbi la umasikini kwa wananchi.
0 Comments