Mkuu wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro , Japhari Kubecha, akizungumza alipokuwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo aliyoifanya Julai 14, 2025 wilayani humo.
.........................................
Na Mwandishi Wetu, Gairo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro , Japhari Kubecha amefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo.
Miradi hiyo imekaguliwa baada ya kufanya vikao vya kukutana na makundi katika wilaya hiyo.
Miradi aliyoitembelea na kuikagua Julai 14, 2025 ipo katika Kata za Gairo ,Msingisi na Rubeho.-
Kwenye ziara hiyo Kubecha alianza kwa kutembelea mradi wa bwalo la Shule ya Sekondari Gairo wenye thamani ya Sh.. Milioni 197 , ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Kata ya Gairo ambao unagharimu Sh.. Milion 528 , ukaguzi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi cha Veta ambao Umegharimu kiasi cha Sh.Bilioni 2 na ukaguzi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari mpya ya Amali ambapo unagharimu Sh. Bilioni 1.6 ,-
Mara baada ya ukaguzi wa miradi hiyo ya maendeleo katika kata hizo, Kubecha ametoa maagizo kuhakikisha miradihiyo hadi ifikapo tarehe 30 Mwezi 8 iwe imekamilika , lakini iwe na ubora na Viwango ambapo alitumia nafasi hiyo kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kueleza kupitia miradi hiyo Wilaya ya Gairo imepokea zaidi ya Bilioni 3 na kuwa hawana deni naye kupitia fedha hizo alizozitoa kwa wilaya hiyo.
Moja ya majengo yaliyokaguliwa.DC Kubecha akipata maelezo wakati wa ziara hiyo.
Maelezo ya mradi huo yakitolewa.
0 Comments