
Na Mwandishi Wetu, Manyara
Mkuu wa Wilaya ya Babati, Mhe. Emanuella Kaganda, amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kuhakikisha anasimamia kwa karibu ujenzi wa Kituo cha Afya Kiru ili ukamilike kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.
Agizo hilo alilitoa wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho kilichpo Kata ya Kiru ambapo alisema Serikali imewekeza fedha nyingi katika sekta ya afya, hivyo ni lazima kila mmoja atimize wajibu wake ili wananchi waepukane na adha ya kufuata huduma za afya umbali wa zaidi ya kilomita 20.
“Nimemuagiza Mkurugenzi kuhakikisha anasimamia ipasavyo kazi hii. Mkandarasi anatakiwa ajenge kwa viwango na ndani ya muda uliopangwa na si vinginevyo,” alisema DC Kaganda.
Katika ziara hiyo, baadhi ya wananchi na watoa huduma wa afya wameeleza kuwa kituo hicho kikikamilika kwa wakati, kitapunguza adha waliyonayo ya upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa kata hiyo na maeneo ya jirani.


0 Comments